Wanaharakati wa kijamii Kenya waahidi kuwatetea watanzania kutafuta haki

Wanaharakati wa kijamii Kenya waahidi kuwatetea watanzania kutafuta haki

Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya yameitaka Serikali ya Tanzania kusikiliza matakwa ya wananchi wake badala ya kuwatishia kukabiliana nao kikamilifu wakati wakipanga kufanya maandamano ya amani.

Wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Vocal Africa Hussein Khalid, Wanaharakati hao walisema watanzania wamekuwa wakiandamana kwa amani na kulilia haki yao lakini serikali ya Tanzania imekuwa ikiwajibu kwa kuwakandama.

Khalid aliwataka watanzania kutorudi nyuma katika kutafuta haki yao, akisema kama watetezi wa haki za kibinadamu katika kanda ya Afrika Mashariki watasimama na watanzania katika kutetea haki yao.

“Sisi kama Watetezi wa haki za kibinadamu tutasimama na watanzania katika kupigania haki yao, na kwamba ni haki ya kila mmoja kuishi kwa amani lakini serikali ya Mama Samia imekuwa ikiwajibu watanzania wanaojitokeza kuandamana kwa amani kwa kuwashambulia na hata wengine kuuwawa”, alisema Khalid.

Kwa upande wake Afisa wa kitengo cha dharura wa Shirika la MUHURI Francis Auma alidai kwamba licha ya kushuhudiwa kwa mauaji nchini Tanzania, serikali ya taifa hilo haijawachukuli sheria waliotekeleza uhalifu huo.

“Ripoti zilionyesha wazi kwamba watu waliouwawa Tanzania ni zaidi ya watu elfu nne na tunashangaa hii serikali ya Mama Samia kwani nini imekosa utu, ni lazima watanzania wapigania haki yao na kukomesha unyanyasaji”, alisema Auma.

Taarifa ya Mwanahabari wetu