Mashirika ya kijamii pwani kuimarisha uwajibikaji sawa na utetezi wa haki

Mashirika ya kijamii pwani kuimarisha uwajibikaji sawa na utetezi wa haki

Mashirika ya kijamii eneo la Pwani yameingia katika mkataba wa makubaliano wa miaka 3 na kamati ya uwajibikaji Mombasa (MAC) unaolenga kuimarisha uwajibikaji, uwazi, na utetezi wa haki za binadamu katika eneo la Pwani.

Kupitia makubaliano hayo, pande hizo mbili zitashirikiana kushughulikia masuala muhimu kama uchambuzi wa sera na sheria, ufuatiliaji wa huduma za umma, ushiriki katika mzunguko wa bajeti, pamoja na kuhimiza uwazi wa matumizi ya fedha za umma.

Mwenyekiti wa muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali Pwani Zedekiah Adika, alisema ushirikiano huo unalenga kuimarisha juhudi za utetezi wa haki na uwajibikaji kwa jamii, akisisitiza kuwa ni muungano wa wadau wenye nia njema kuhakikisha kaunti na taifa linaongozwa kwa misingi ya uwazi na uwajibikaji.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa MAC, Kassim Ziro, alisema ni wakati wa vyama vya wafanyakazi kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii, kwani changamoto za huduma za umma pia zinawaathiri wafanyakazi kila siku.

Taarifa Mwanahabari wetu.