Wakenya 15 kufurushwa nchini Marekani

Wakenya 15 kufurushwa nchini Marekani

Serikali ya Marekani imetoa orodha ya wakenya 15 ambao watafurushwa nchini humo.

Wakenya hawa ni wale waliokabiliwa na kesi mbalimbali ikiwemo wizi wa mabavu, ulanguzi wa dawa za kulevya na hata wengine kwa kuendesha gari wakiwa walevi.

Hii ni sehemu ya awamu ya serikali ya rais Donald Trump kuwaondoa watu inaowataja kuwa ‘wageni wabaya.

Majina ya wakenya hao yalichapishwa kwenye tovuti ya umma ilioanzishwa na idara ya usalama wa Marekani inayoonyesha waliolengwa.

Miongoni mwa wakenya hao ni Alfred Obiero mkaazi wa jimbo la Colorado ambaye alipatikana na hatia ya kushambulia, kuendesha gari akiwa mlevi na ukatili wa nyumbani.

Wengine ni pamoja na Bethwel Gathu, Patrick Mwangi, Daniel Kathuu, Mohammed Chepchekani, Moffat Mureithi, Francis Mungai, Anthoni Karia miongoni mwa wengine.

Taarifa kutoka Marekani ilionyesha kuwa kuna wakenya 1,282 wanaoishi Marekani ambao wanalengwa kufurushwa, huku kundi la kwanza la wakenya 15 likiwa limeondoka tarehe 15 mwezi juni mwaka huu.

Taarifa ya Joseph Jira