Magavana waishtumu Wizara ya afya nchini kwa kutoshirikiana na serikali za kaunti

Magavana waishtumu Wizara ya afya nchini kwa kutoshirikiana na serikali za kaunti

Mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Ahmed Abdillahi ameishtumu Wizara ya afya nchini kwa kutoshirikiana na serikali za kaunti katika utekelezaji wa bima ya afya ya jamii SHA.

Abdillahi ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Wajir, alisema ni lazima serikali iweke mikakati bora zaidi ya kulinda serikali za ugatuzi kwani zinamchanga mkubwa katika kufanikisha maendeleo ya wananchi mashinani.

Wakizungumza katika eneo la Naivasha wakati wa Kongamano la Afya, Magavana walisema Wizara ya Afya inaingilia majukumu ya serikali za kaunti na kuvurugu mpango wa SHA.

Magavana hao walisema muingiliano huo wa majukumu kwenye sekta ya afya, kumechangia kucheleweshwa malipo kwa hospitali zinazotoa huduma za afya kupitia mpango wa SHA.

Kwa upande wake Waziri wa Afya nchini Aden Duale alisema Wizara yake inaangazia upya mbinu ya kuongeza mgao wa fedha inazilipa.