Tume ya uchaguzi nchini Cameroon imemtangaza Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 92 kama mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais uliyofanyika Oktaba 12 mwaka huu.
Biya alishindi uchaguzi huo kwa kupata asilimia 53.7 ya kura zilizopigwa huku mpinzani wake wa karibu Issah Tchiroma akipata asilimia 35.2.
Biya anachukua hatamu ya uongozi kwa muhula wa wanane ambayo inajumuisha miaka 43 ya utawala, tangu alipoingia madarakani mwaka 1982.
Kutangazwa Rais Paul Biya kuwa mshindi wa uchaguzi huo kulisababisha vurugu, ghasia na machafuko nchini humo na kusababisha watu wanne kupoteza maisha yao baada yaku pigwa risasi na maafisa wa kukabiliana na ghasia.
Mchafuko hayo yametokana na shinikizo kutoka kwa raia wanamtaka Biya ajiuzulu kama rais wa taifa hilo la Afrika magharibi, kwani shinikizo kama hizo zimetolewa na mpinzani wake wa karibu wa kisiasa Issa Tchiroma ambaye alidai kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na wizi wa kura.
