Beldine Odemba ameahidi wana Mortisha Kushinda na kufuzu Kombe la AWCON mwaka 2027

Beldine Odemba ameahidi wana Mortisha Kushinda na kufuzu Kombe la AWCON mwaka 2027

Kocha mkuu wa Harambee Starlets, Beldine Odemba, amesema kuwa motisha ya kifedha iliyotolewa na Rais William Ruto itakuwa na mchango mkubwa wa kisaikolojia kwa wachezaji wake wanapolenga kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.

Starlets wako dakika 90 pekee — mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumanne jioni — kufuzu kwa fainali za WAFCON zitakazofanyika nchini Morocco mwaka ujao.

Rais Ruto aliwazawadia Starlets jumla ya KSh 10 milioni kufuatia ushindi wao wa 3–1 dhidi ya The Gambia katika mchezo wa kufuzu uliochezwa Ijumaa jioni kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi.

Kiongozi wa Taifa awali alikuwa amewapa KSh 5 milioni kama motisha kabla ya mechi na kuongeza KSh 5 milioni kwa ushindi wa nyumbani. Aidha, aliahidi KSh 1 milioni kwa kila mchezaji iwapo timu itashinda na kufuzu, na KSh 500,000 kila mmoja iwapo watatoka sare.

“Haikuwa sehemu ya maandalizi, lakini bila shaka motisha huleta athari chanya kwa timu. Wachezaji hupenda kucheza kwa ajili ya kitu, na wakipewa ahadi kutoka kwa 001 (Rais), wanapata hamasa zaidi,” alisema Odemba.

Starlets watacheza mchezo wa marudiano dhidi ya The Gambia Jumanne katika Uwanja wa Stade Lat Dior huko Thies, Senegal, baada ya Gambia kukosa uwanja uliothibitishwa na FIFA. Odemba alisema hali hiyo ni faida kubwa kwa upande wa Kenya.

“Ili kuwa bingwa, lazima uwe na wachezaji mabingwa kwenye kikosi chako. Tumewajumuisha wachezaji watatu waliocheza WAFCON 2016, jambo ambalo ni motisha kubwa kwa wengine. Wamekuwa wakizungumza kuhusu umuhimu wa kufuzu na wako tayari kufanya hivyo kwa mara ya pili,” aliongeza kocha huyo.

Sare ya aina yoyote itatosha kupeleka kikosi cha Beldine Odemba kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba.

Toleo la mwaka 2026 la WAFCON litafanyika nchini Morocco kuanzia Machi 17 hadi Aprili 3.