Kiongozi wa Chama Cha CHADEMA Tundu Lissu ametoa taarifa kuelezea hofu dhidi ya maisha yake,kufuatia hatua ya serikali na maafisa wa Gereza la Ukonga anakozuiliwa Lissu, ya kumhamishia chemba inayomtenga kabisa na wafungwa wengine wanakabiliwa na mashtaka ambayo adhabu yake ni Kifo.
Lissu anaitaja hatua hiyo kuwa ‘upweke wa kulazimishwa’
“Wafungwa wenzangu waliokuwa nami kwenye seli moja, ambao walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, wametolewa wote nimeachwa peke yangu,”Akasema Lissu.

Tundu Lissu akiwa kotini
Taarifa hiyo inaongeza kuwa seli hiyo imewekwa kamera za CCTV kurekodi kila kitu kinachoendelea selini humo, ikiwa ni pamoja na wakati anapobadilisha nguo au kujisaidia, hali inayomtia hofu zaidi kiongozi huyo wa CHADEMA.
“Sina faragha yoyote tena, na wala hili sio tena suala la usalama bali ni kudhalilishwa kwa utu wangu kama binadamu.” Akiongeza kusema Tundu Lissu.
Chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 12 na 13, zinazolinda hadhi ya mfungwa ni kinyume Cha Sheria na ukiukaji WA haki kupitia kuteswa au kudhalilishwa kwa mfungwa gerezani.
