Mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini Aisha Jumwa amekosoa matamshi ya viongozi wa chama cha ODM ya kujitenga na uhusiano wao na serikali jumuishi katika kampeni za chaguzi ndogo sehemu mbali mbali nchini.
Jumwa alisema matamshi hayo yanakiuka mkataba ambao ulikuwa umeafikiwa baina ya kinara wa chama hicho hayati Raila Odinga na rais William Ruto.
Kulingana na Jumwa, makubaliano ya vyama hivyo kutosimamisha wagombea katika baadhi ya maeneo kwenye chaguzi hizo ndogo haimaanishi kwamba vilikuwa dhaifu, bali ni kushirikiana baada ya maafikiano hayo ya serikali jumuishi kuhakikisha wanapata ushindi.
Viongozi wa chama cha ODM wakiongozwa na mwakilishi wa kike kaunti ya Kisumu Ruth Odinga, walisema chama hicho kinafanya kampeni zake binafsi na kwamba hakitambui chama kinachoitwa broadbased.
Tarifa ya Joseph Jira
