Maelfu ya vijana wajitokeza kwa mradi wa NYOTA kaunti ya Kilifi

Maelfu ya vijana wajitokeza kwa mradi wa NYOTA kaunti ya Kilifi

Maelfu ya vijana kutoka wadi mbalimbali eneo bunge la Kilifi kazkazini kaunti ya Kilifi wamehudhuria zoezi la kutibitisha majina ya wale waliofaulu katika mradi wa NYOTA.

Akizungumza na Wanahabari baada ya zoezi hilo, Katibu wa Wizara ya vijana nchini Fikirini Jacobs alisema mradi huo umelenga vijana 70 kwa kila wadi ambao watapokea shilingi elfu 50 kwa kila kijana ili kuanzisha biashara.

Jacobs aliongezea kwamba mradi huo utakaogharimu shilingi bilioni 20, unalenga vijana ambao walikosa nafasi za kuendeleza masomo yao baada ya kukamilisha kidato cha nne na darasa la 8 ambao bado wako chini ya umri wa miaka miaka 29.

“Huu mradi unalenga kuhakikisha vijana wa umri wa miaka 18 hadi 29 wananufaika na fedha hizi na zitapeanwa kuwa vijana na kila mmoja atapata shilingi elfu 50 za kuwasaidia,” alisema Fikirini.

Naye Naibu Kamishena wa eneo hilo Samuel Mutisya, aliwahimiza vijana kuchukua vitambulisho ili wasipitwe na nafasi za ajira zilizotangazwa na serikalini.

Kwa upande wao vijana waliohudhuria zoezi hilo wakiongozwa na Peter mweni, wameusifu mradi huo, wakisema utawasaidia kimaisha, japo wameitaka serikali kujumuisha vijana wote kwani kuwa wale waliosoma lakini hawana ajira.