Hospitali ya Rufaa ya kaunti ya Kilifi imepata mafanikio ya kihistoria ya kitabibu baada ya kufanikisha uzalishaji watoto mapacha walioshikana kwa mara ya kwanza.
Watoto hao mapacha ambao walioshikana katika sehemu ya tumbo, wako katika hali salama pamoja na mama yao kwani shughuli hiyo ya uzalishaji ilifanywa kwa ustadi wa hali ya juu.
Wataalamu wa kiafya walifanikisha uzalishaji huo wa watoto mapacha walioshikana ni pamoja na Daktari Sumeiya wa magonjwa ya Wanawake, Daktari Kadivani wa upasuaji wa watoto, Daktari Kalama wa kuhudumia watoto pamoja na usaidizi wa wauguzi wa wodi za uzazi.
Daktari mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya kaunti ya Kilifi, Dkt. Gilbert Angore, waliwapongeza madaktari waliofanikisha shughuli hiyo, akisema Mama na watoto hao wako katika hali nzuri na watasafirishwa hadi Hospitali kuu ya kitaifa ya Kenyatta jijini Nairobi kwa uangalizi zaidi.

Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya kaunti ya Kilifi wakiongozwa na Daktari mkuu Gilbert Angore wakiwa na Jemimah Sidi Nzai ambaye ni mama wa mapacha walioshikana
Hata hivyo mama wa watoto hao Jemimah Sidi Nzai alielezea jinsi alivyopokea matibabu hadi ya kujifungua watoto hao mapacha walioshikana, akielezea matumani yake ya kupata matibabu zaidi katika hospitali kitaifa ya Kenyatta jijini Nairobi
