Bei za baadhi ya bidhaa humu nchini zinatarajiwa kupanda hata zaidi msimu huu ikilinganishwa na hapo awali.
Wafanyibiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nchi jirani Tanzania mjini Kilifi walisema bidhaa kama vile kitunguu zinatarajwa kupanda bei kutokana na maandamano ambayo yalishuhudiwa hivi karibuni.
Kulingana na wafanyibiashara hao hali ilivyo kwa sasa katika taifa la Tanzania hawawezi kuingia katika taifa hilo kununua na hata kuangiza bidhaa kutoka nchi hiyo.
Kwa sasa kilo ya kitunguu inauzwa kwa shilingi 100 katika soko la Kwa Charo wa mae mjini Kilifi sawa na soko la mazeras kaunti ya Kilifi bei ambayo inatarajiwa kupanda.
Hata hivyo walitolea wito wakulima wa humu nchini kuendeleza kilimo cha Kitunguu kwa wingi ili kukoma kutengemea Kitunguu kutoka nchi jirani ya Tanzania.
“Biashara inatarajiwa kuwa ngumu kwani kupata bidhaa ambazo tunatarajia kutoa Tanzania itakuwa ngumu kwani wengi wanaogopa kuingia katika nchini hiyo.
‘”Wakulima wa humu nchini lazima waongeze kiwango cha kitunguu wanachopanda ili kusaidia hali hii”.
Taarifa ya Pauline Ngome
