Shirika la APDK na CocoFm watoa ufadhili wa vifaa kwa watoto walemavu

Shirika la APDK na CocoFm watoa ufadhili wa vifaa kwa watoto walemavu

Tabasamu na matumaini zimetanda miongoni mwa familia za watoto wenye uwezo maalum mjini Kilifi baada ya Shirika la Association for the Physically Disabled of Kenya kwa ushirikiano na Coco FM kukabidhi vifaa maalum vya mazoezi kwa watoto 10 wenye uwezo maalum.

Hatua hii inalenga kuboresha afya na maisha yao ya kila siku kufuatia mahitaji yaliyoibuliwa wakati wa kambi ya matibabu iliyoandaliwa na CocoFm mwezi Oktoba na Novemba mwaka 2025.

Wazazi wa watoto wenye ulemavu wa viungo walipokea vifaa vya kuwasaidia watoto wao.

Katika halfa ndogo iliyofanika katika Ofisi za CocoFm, wazazi na watoto waliotambulika kupokea vifaa hivyo walifika ili kupata ufadhili huo na kushughulikiwa na wahudumu wa Shirika la APDK, pamoja na kupewa vifaa maalumu vya mazoezi vya watoto hao.

Afisa wa Shirika la APDK Walter Luvai akiwaleza wazazi wa watoto wenye ulemavu jinsi ya kutumia vifaa hivyo vya matibabu

Wazazi hao waliozungumza kuhusu safari yao ya maisha na watoto hawa.

Walikabidhiwa vifaa maalumu vya kuwasaidia watoto wao.

Walielezea shukran zao kwa msaada huo, wakisema umeleta matumaini mapya kwa familia zao.

Meneja wa kituo cha habari cha Coco FM Said Kashindo, alisisitiza dhamira ya kituo cha CocoFm kuandaa kambi zaidi za matibabu, ili kuendelea kuwafikia na kuwahudumia wasikilizaji wa CocoFM walio na changamoto mbalimbali za kiafya.

Shughuli hii inafuatia Kambi ya matibabu iliyoandaliwa mwaka uliopita.

Taarifa ya Lolani Kalu